Mafanikio katika maisha huja kwa bidii ya mtu katika jambo/mambo ayafanyayo. Hii inajidhihirisha katika jamii zetu, pengine kwa kuona maisha ya mtu yanavyobadilika. Na umri mzuri wa kupata mafanikio ni katika ujana, ili kuandaa mazingira mazuri uzeeni.


Baadhi ya mambo niliyo kutana nayo kwa wazee, wazazi na vijana wenzetu juu ya mafanikio ni haya;

  • Weka malengo yako, na mtambue/mtafute mtu (Role model) anaekupa hamasa katika kutafuta mafanikio.
  • Watu hawafanikishi mambo makubwa kwa wakati mmoja(haraka na ghafla); bali kwa kuweka malengo madogo madogo kwa muda mfupi na kuyatimiza.
  • Soma na ujifunze maisha ya watu waliofanikiwa katika jamii yako na nje yake pia.
  • Njia rahisi ya kuwa tajiri/mwenye mali ni kutumia kipaji na uhodari wako kwa yale unayoyajua na kuyaweza.
  • Mawasiliano yako baina ya watu huleta mafanikio kwa kuongeza wigo wako wa kujua na kujulikana kwa watu.
  • Ni muda wa kuongeza kipato chako kwa kuwekeza hela zako.
  • Ongeza jitihada katika kile ukifanyacho sasa, ili kuona matokeo yake.
  • Ni muda mzuri wa kuwa mjasiriamali kwa kua bado una muda na nguvu. 
  • Ili kutajirika mapema katika ujana, yakubidi uwe benki ya uwekezaji (kukopesha watu ama vikundi).
  • Soko la hisa ni njia nzuri ya kutajirika katika umri mdogo. Lakini pata elimu yake kwanza kabla ya kujaribu.
  • Jitahidi kuwekeza katika rasilimali zenye thamani.
  •  

    Hayo ni baadhi ya mambo machache yanayoweza kusaidia kufikia mafanikio yako maishani.

    Kwa habari kama hizi na zinginezo, fuatilia blogu yangu hii.